8 Mwezi wa tano: Shamhuthi, Mwizrahi; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
9 Mwezi wa sita: Ira, mwana wa Ikeshi, Mtekoa; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
10 Mwezi wa saba: Helesi, Mpeloni, wa wana wa Efraimu; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
11 Mwezi wa nane: Sibekai, Mhushathi, wa Wazera; alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
12 Mwezi wa tisa: Abiezeri Mwanathothi, wa Wabenyamini; naye alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
13 Mwezi wa kumi: Maharai, Mnetofathi wa Wazera; naye alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.
14 Mwezi wa kumi na moja: Benaya, Mpirathoni; wa wana wa Efraimu, naye alikuwa na kundi la wanajeshi 24,000.