1 Hawa ndio wana wa mfalme Daudi waliozaliwa wakati alipokuwa huko Hebroni:Amnoni, mzaliwa wake wa kwanza; mama yake aliitwa Ahinoamu, Myezreeli; wa pili Danieli ambaye mama yake alikuwa Abigaili, Mkarmeli;
2 wa tatu alikuwa Absalomu, ambaye mama yake alikuwa Maaka, bintiye Talmai mfalme wa Geshuri; wa nne alikuwa Adoniya, ambaye mama yake alikuwa Hagithi;
3 wa tano alikuwa Shefatia, ambaye mama yake alikuwa Abitali; na wa sita alikuwa Ithreamu, ambaye mama yake alikuwa Egla.
4 Wote sita, walizaliwa Hebroni ambako Daudi alitawala kwa muda wa miaka saba na nusu. Huko Yerusalemu, alitawala kwa muda wa miaka thelathini na mitatu.
5 Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6 Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti,
7 Noga, Nefegi, Yafia,