14 aliyemzaa Amoni, aliyemzaa Yosia.
15 Yosia alikuwa na wana wanne: Yohanani, mzaliwa wake wa kwanza, wa pili Yehoyakimu, wa tatu Sedekia na wa nne Shalumu.
16 Yehoyakimu alikuwa na wana wawili: Yekonia na Sedekia.
17 Wana wa Yekonia aliyechukuliwa mateka na Wababuloni walikuwa saba: Shealtieli,
18 Malkiramu, Pedaya, Shenazari, Yekamia, Hoshama na Nedabia.
19 Wana wa Pedaya walikuwa Zerubabeli na Shimei. Zerubabeli alikuwa na wana wawili: Meshulamu na Hanania, na binti mmoja, jina lake Shelomithi.
20 Zerubabeli pia alikuwa na wana wengine watano: Hashuba, Oheli, Berekia, Hasadia na Yushab-hesedi.