4 Wote sita, walizaliwa Hebroni ambako Daudi alitawala kwa muda wa miaka saba na nusu. Huko Yerusalemu, alitawala kwa muda wa miaka thelathini na mitatu.
5 Wafuatao ni wana wa mfalme Daudi alipokuwa Yerusalemu: Mkewe Bathshua, bintiye Amieli, alimzalia wana wanne: Himea, Shobabu, Nathani na Solomoni.
6 Na mbali na hao alikuwa na wana wengine tisa: Ibhari, Elishua, Elifaleti,
7 Noga, Nefegi, Yafia,
8 Elishama, Eliada na Elifeleti.
9 Hao wote walikuwa wana wa Daudi, mbali na wale wengine waliozaliwa na masuria wake. Daudi alikuwa na binti pia, aliyeitwa Tamari.
10 Wazawa wa mfalme Solomoni: Solomoni alimzaa Rehoboamu, aliyemzaa Abiya, aliyemzaa Asa, aliyemzaa Yehoshafati,