32 Pia, waliishi katika miji mingine mitano: Etamu, Aini, Rimoni, Tokeni na Ashani,
33 pamoja na vijiji kandokando ya miji hiyo huko Baali. Hayo ndiyo yaliyokuwa makao yao, nao waliweka kumbukumbu ya nasaba yao.
34 Watu wafuatao walikuwa wakuu wa koo zao: Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,
35 Yoeli, Yehu (mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.)
36 Eliehonai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,
37 Ziza (mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri na mwana wa Shemaya).
38 Jamaa zao waliendelea kuongezeka kwa wingi sana. Hawa waliotajwa majina ni wakuu katika jamaa zao na koo zao ziliongezeka sana.