34 Watu wafuatao walikuwa wakuu wa koo zao: Meshobabu, Yamleki, Yosha mwana wa Amazia,
35 Yoeli, Yehu (mwana wa Yoshibia, mwana wa Seraya, mwana wa Asieli.)
36 Eliehonai, Yaakoba, Yeshohaya, Asaya, Adieli, Yesimieli, Benaya,
37 Ziza (mwana wa Shifi, mwana wa Aloni, mwana wa Yedaya, mwana wa Shimri na mwana wa Shemaya).
38 Jamaa zao waliendelea kuongezeka kwa wingi sana. Hawa waliotajwa majina ni wakuu katika jamaa zao na koo zao ziliongezeka sana.
39 Walienea hadi kwenye lango la mji wa Gedori, upande wa mashariki wa bonde, ili kuwatafutia kondoo wao malisho.
40 Hapo, walipata malisho tele, tena mazuri sana na pia nchi ilikuwa wazi, tulivu na yenye amani, kwani wenyeji wa nchi hiyo wa hapo awali walikuwa Wahamu.