5 Mika, Reaya, Baali,
6 na Beera, ambaye mfalme Tiglath-pileseri wa Ashuru, alimchukua mateka ingawa alikuwa kiongozi wa Wareubeni, akampeleka uhamishoni.
7 Wakuu wa koo wafuatao waliandikishwa katika orodha ya kumbukumbu ya kabila la Reubeni, Yeieli, Zekaria,
8 Bela, mwana wa Azazi na mjukuu wa Shema, wa ukoo wa Yoeli, uliokuwa ukiishi Aroeri na katika eneo lote la kaskazini hadi Bela na Baal-meoni.
9 Pia, kwa maana mifugo yao iliongezeka kwa wingi sana, walisambaa upande wa mashariki hadi kwenye maingilio ya jangwa lililoenea hadi mto Eufrate.
10 Katika siku za mfalme Shauli, kabila la Reubeni lilizusha vita dhidi ya Wahajiri, wakawaua vitani na kuitwaa ardhi yao yote mashariki mwa Gileadi, wakaishi humo.
11 Kabila la Gadi lilipakana na kabila la Reubeni upande wa kaskazini, katika nchi ya Bashani iliyoenea mashariki hadi Saleka.