54 Yafuatayo ndiyo makazi yao kulingana na mipaka yake: Wazawa wa Aroni katika jamaa ya Wakohathi kulingana na kura yao,
55 hao walipewa mji wa Hebroni katika nchi ya Yuda na malisho kandokando yake.
56 Lakini mashamba ya mjini pamoja na malisho yake alipewa Kalebu mwana wa Yefune.
57 Wazawa wa Aroni walipewa miji ya makimbilio: Hebroni, Libna pamoja na malisho yake, Yatiri na Eshtemoa pamoja na malisho yake,
58 Hileni na Debiri pamoja na malisho yake,
59 Ashani na Beth-shemeshi pamoja na malisho yake.
60 Katika eneo la kabila la Benyamini walipewa miji ya Geba, Alemethi na Anathothi pamoja na malisho ya miji hiyo. Miji yote waliyopewa kulingana na jamaa zao ilikuwa kumi na mitatu.