29 Yeieli, alikuwa mwanzilishi wa mji wa Gibeoni. Mkewe alikuwa Maaka.
30 Mzaliwa wake wa kwanza alikuwa Abdoni. Wanawe wengine ni Zuri, Kishi, Baali, Nadabu,
31 Gedori, Ahio, Zekeri,
32 na Miklothi baba yake Shimea. Hawa pia waliishi Yerusalemu karibu na watu wengine wa ukoo wao.
33 Neri alimzaa Kishi, Kishi akamzaa Shauli. Shauli alikuwa na wana wanne: Yonathani, Malki-shua, Abinadabu na Eshbaali.
34 Yonathani alimzaa Merib-baali, na Merib-baali akamzaa Mika.
35 Mika alikuwa na wana wanne: Pithoni, Meleki, Terea na Ahazi.