54 Daudi alikichukua kichwa cha yule Goliathi, Mfilisti, akakipeleka mjini Yerusalemu. Lakini silaha za Goliathi akaziweka katika hema lake.
55 Shauli alipomwona Daudi akienda kumkabili yule Mfilisti Goliathi, alimwuliza Abneri, kamanda wa jeshi lake, “Abneri, huyu ni kijana wa nani?” Abneri alijibu, “Mfalme, kama uishivyo, mimi sijui.”
56 Mfalme Shauli akamwambia, “Basi, uliza yeye ni kijana wa nani.”
57 Mara tu Daudi aliporudi kambini baada ya kumuua Goliathi, Abneri alimchukua na kumpeleka kwa Shauli. Wakati huo Daudi alikuwa bado amechukua kichwa cha Goliathi mikononi mwake.
58 Shauli akamwuliza Daudi, “Kijana, wewe ni mwana wa nani?” Daudi akajibu, “Mimi ni mwana wa mtumishi wako Yese, kutoka mji wa Bethlehemu.”