1 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Moabu wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamemkosea heshima marehemu mfalme wa Edomukwa kuichoma moto mifupa yakeili kujitengenezea chokaa!
2 Basi, nitaishushia moto nchi ya Moabu,na kuziteketeza kabisa ngome za mji wa Keriothi.Wanajeshi watakapopaza sauti zao na kupiga tarumbeta,watu wa Moabu watakufa katika makelele hayo ya vita.
3 Isitoshe, nitamuua mtawala wa Moabu,pamoja na viongozi wote wa nchi hiyo.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”
4 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu wa Yuda wametenda dhambi tena na tena,kwa hiyo sitaacha kuwaadhibu.Wamepuuza sheria zangu,wala hawakufuata amri zangu.Wamepotoshwa na miungu ileile waliyoihudumia wazee wao.