Amosi 5 BHN

Maombolezo ya Amosi

1 Sikilizeni maombolezo yangu juu yenu,enyi Waisraeli:

2 Umeanguka na hutainuka tenaewe binti Israeli!Umeachwa pweke nchini mwako,hamna hata mtu wa kukuinua.

3 Maana Bwana Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu 1,000 watatoka mjini kwenda kupiganalakini watarejea 100 tu;wataondoka watu 100 wa kijiji kimojalakini watanusurika watu kumi tu.”

4 Mwenyezi-Mungu awaambia hivi Waisraeli:“Nitafuteni mimi nanyi mtaishi!

5 Lakini msinitafute huko Betheliwala msiende Gilgaliwala msivuke kwenda Beer-sheba.Maana wakazi wa Gilgali,hakika watachukuliwa uhamishoni,na Betheli utaangamizwa!”

6 Mtafuteni Mwenyezi-Mungu, nanyi mtaishi!La sivyo, atawalipukia wazawa wa Yosefu kama moto;moto utawateketeza wakazi wa Bethelina hakuna mtu atakayeweza kuuzima.

7 Tahadhari enyi mnaogeuza haki kuwa uchungu,na kuuona uadilifu kuwa kama takataka!

8 Huyo aliyezifanya Kilimia na sayari Orioni,ambaye huligeuza giza nene kuwa mchana,na mchana kuwa usiku;yeye ambaye ayaitaye pamoja maji ya baharina kuyamwaga juu ya nchi kavu,Mwenyezi-Mungu ndilo jina lake.

9 Yeye ndiye anayewaangamiza wenye nguvu,na kuziharibu ngome zao.

10 Nyinyi huwachukia watetezi wa hakina wenye kusema ukweli mahakamani.

11 Nyinyi mnawakandamiza fukarana kuwatoza kodi ya ngano kupita kiasi.Mnajijengea nyumba za mawe ya kuchonga,lakini nyinyi hamtaishi humo;mnalima bustani nzuri za mizabibu,lakini hamtakunywa divai yake.

12 Maana mimi najua wingi wa makosa yenuna ukubwa wa dhambi zenu;nyinyi mnawatesa watu wema,mnapokea rushwana kuzuia fukara wasipate haki mahakamani.

13 Basi, kutakuwa na wakati mbayaambao hata mwenye busara atanyamaza.

14 Tafuteni kutenda mema na si mabaya,ili nyinyi mpate kuishinaye Mwenyezi-Mungu wa majeshiawe pamoja nanyi kama mnavyosema.

15 Chukieni uovu, pendeni wema,na kudumisha haki mahakamani.Yamkini Mwenyezi-Mungu wa majeshi atawafadhili watu wa Yosefu waliobaki.

16 Basi, Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi,naam, Mwenyezi-Mungu asema:“Patakuwa na kilio kila mahali mitaani;watu wataomboleza: ‘Ole! Ole!’Wakulima wataitwa waje kuomboleza,na mabingwa wa kuomboleza waje kufanya matanga.

17 Patakuwa na kilio katika mashamba yote ya mizabibu;maana nitapita kati yenu kuwaadhibu.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.”

Siku ya Mwenyezi-Mungu

18 Ole wenu nyinyi mnaoingojea kwa hamusiku ya Mwenyezi-Mungu!Kwa nini mnaitaka sana siku hiyo?Siku hiyo, itakuwa siku ya giza na sio ya mwanga!

19 Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba,halafu akakumbana na dubu!Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake,akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.

20 Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;itakuwa huzuni bila uangavu wowote.

21 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nazichukia na kuzidharau sikukuu zenu;siifurahii mikutano yenu ya kidini.

22 Mjaponitolea sadaka zenu za kuteketezwa na za nafaka,mimi sitakubali kuzipokea;na sadaka zenu za amani za wanyama wanonomimi sitaziangalia kabisa.

23 Ondoeni mbele yangu kelele za nyimbo zenu!Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!

24 Lakini acheni haki itiririke kama maji,uadilifu uwe kama mto usiokauka.

25 “Enyi Waisraeli, wakati ule mlipokuwa kule jangwani kwa miaka arubaini, je, mliniletea tambiko na sadaka hata mara moja?

26 Je, wakati huo mlibeba kama sasa vinyago vya mungu wenu Sakuthi mfalme wenu na vinyago vya Kaiwani mungu wenu wa nyota, vitu ambavyo mlijitengenezea wenyewe?

27 Kwa hiyo nitawapeleka uhamishoni, mbali kuliko Damasko! Hayo amesema Mwenyezi-Mungu, ambaye jina lake ni Mungu wa Majeshi.

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9