Amosi 4 BHN

1 Sikilizeni neno hili,enyi wanawake ng'ombe wa Bashanimlioko huko mlimani Samaria;nyinyi mnaowaonea wanyonge,mnaowakandamiza maskini,na kuwaambia waume zenu:“Tuleteeni divai tunywe!”Sikilizeni ujumbe huu:

2 Mimi Bwana Mwenyezi-Mungu Mtakatifu nimeapa:“Tazama, siku zaja,ambapo watu watawakokoteni kwa kulabu,kila mmoja wenu kama samaki kwenye ndoana.

3 Mtaburutwa hadi ukutani palipobomolewa,na kutupwa nje.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

Israeli haijajirekebisha bado

4 “Enyi Waisraeli,nendeni basi huko Betheli mkaniasi!Nendeni Gilgali mkalimbikize makosa yenu!Toeni sadaka zenu kila asubuhi,na zaka zenu kila siku ya tatu.

5 Toeni tambiko ya shukrani ya mikate iliyochachushwa.Tangazeni popote kwamba mmetoa kwa hiari;kwani ndivyo mnavyopenda kufanya!Mimi Bwana Mungu nimenena.

6 “Mimi niliwanyima chochote cha kutafuna,nikasababisha ukosefu wa chakula popote.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

7 “Tena niliwanyima mvuamiezi mitatu tu kabla ya mavuno.Niliunyeshea mvua mji mmoja,na mji mwingine nikaunyima.Shamba moja lilipata mvua,na lingine halikupata, likakauka.

8 Watu wa miji miwili, mitatu wakakimbilia mji mwingine,wapate maji, lakini hayakuwatosha.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

9 “Niliwapiga pigo la ukame na ukungu;nikakausha bustani na mashamba yenu ya mizabibu;nzige wakala mitini na mizeituni yenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

10 “Niliwaleteeni ugonjwa wa taunikama ule nilioupelekea Misri.Niliwaua vijana wenu vitani,nikawachukua farasi wenu wa vita.Maiti zilijaa katika kambi zenu,uvundo wake ukajaa katika pua zenu.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

11 “Niliwaangusha baadhi yenu kwa maangamizikama nilivyoangamiza Sodoma na Gomora.Wale walionusurika miongoni mwenu,walikuwa kama kijiti kilichookolewa motoni.Hata hivyo hamkunirudia.Nasema mimi Mwenyezi-Mungu.

12 “Kwa hiyo, enyi Waisraeli, nitawaadhibu.Na kwa kuwa nitafanya jambo hilo,kaeni tayari kuikabili hukumu yangu!”

13 Mungu ndiye aliyeifanya milima,na kuumba upepo;ndiye amjulishaye mwanadamu mawazo yake;ndiye ageuzaye mchana kuwa usiku,na kukanyaga vilele vya dunia.Mwenyezi-Mungu wa Majeshi ndilo jina lake!

Sura

1 2 3 4 5 6 7 8 9