12 Mwenyezi-Mungu, asema hivi: “Kama vile mchungaji ampokonyavyo simba kinywani miguu miwili tu au kipande cha sikio la kondoo, ndivyo watakavyonusurika watu wachache tu wa Israeli wakaao Samaria, ambao sasa wanalalia vitanda vizuri na matandiko ya hariri.”
13 Bwana Mungu wa majeshi asema hivi:“Sikilizeni, mkawaonye wazawa wa Yakobo:
14 Siku nitakapowaadhibu Waisraelikwa sababu ya makosa yao,nitayaharibu pia madhabahu ya mji wa Betheli.Nitazikata pembe za kila madhabahuna kuziangusha chini.
15 Nitaziharibu nyumba zote mjini na vijijini;nitazibomoa nyumba zilizopambwa kwa pembe,majumba makubwamakubwa hayatasalia hata moja.Mimi Mwenyezi-Mungu nimesema.”