5 Je, mtego bila chamboutamnasa ndege?Je, mtego hufyatukabila kuguswa na kitu?
6 Je, baragumu ya vita hulia mjinibila kutia watu hofu?Je, mji hupatwa na jangaasilolileta Mungu?
7 Hakika, Bwana Mwenyezi-Mungu hafanyi kitubila kuwafunulia watumishi wake manabii nia yake.
8 Simba akinguruma,ni nani asiyeogopa?Bwana Mwenyezi-Mungu akinena,ni nani atakataa kuutangaza ujumbe wake?
9 Tangazeni katika ikulu za Ashdodi,na katika ikulu za nchi ya Misri:“Kusanyikeni kwenye milimainayoizunguka nchi ya Samaria,mkajionee msukosuko mkubwana dhuluma zinazofanyika humo.”
10 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Watu hawa wameyajaza majumba yaovitu vya wizi na unyang'anyi.Hawajui kabisa kutenda yaliyo sawa!
11 Kwa hiyo, adui ataizingira nchi yao,atapaharibu mahali pao pa kujihami,na kuziteka nyara ikulu zao.”