19 Mambo yatakuwa kama mtu aliyekimbia simba,halafu akakumbana na dubu!Au kama mtu anayerudi nyumbani kwake,akatia mkono ukutani, akaumwa na nyoka.
20 Siku ya Mwenyezi-Mungu itakuwa giza, na sio mwanga;itakuwa huzuni bila uangavu wowote.
21 Mwenyezi-Mungu asema hivi:“Nazichukia na kuzidharau sikukuu zenu;siifurahii mikutano yenu ya kidini.
22 Mjaponitolea sadaka zenu za kuteketezwa na za nafaka,mimi sitakubali kuzipokea;na sadaka zenu za amani za wanyama wanonomimi sitaziangalia kabisa.
23 Ondoeni mbele yangu kelele za nyimbo zenu!Sitaki kusikiliza muziki wa vinubi vyenu!
24 Lakini acheni haki itiririke kama maji,uadilifu uwe kama mto usiokauka.
25 “Enyi Waisraeli, wakati ule mlipokuwa kule jangwani kwa miaka arubaini, je, mliniletea tambiko na sadaka hata mara moja?