5 Nyinyi mnapenda kuimba ovyo na sauti ya vinubina kubuni ala mpya za muziki mkimwiga mfalme Daudi.
6 Mnakunywa divai kwa mabakuli,na kujipaka marashi mazuri mno.Lakini hamhuzuniki hata kidogojuu ya kuangamia kwa wazawa wa Yosefu.
7 Kwa hiyo mtakuwa wa kwanza kwenda uhamishoni,na karamu za wenye kustarehe zitatoweka.
8 Bwana Mwenyezi-Mungu ameapa kwa nafsi yake;Mwenyezi-Mungu, Mungu wa majeshi asema:“Nachukizwa mno na kiburi cha wazawa wa Yakobo;tena nayachukia majumba yao ya fahari.Mji wao na vyote vilivyomo nitawapa adui zao.”
9 Kama wakibaki watu kumi katika nyumba moja, wote watakufa.
10 Na atakapokuja mjomba wa aliyekufa kuitoa maiti nje aichome, akamwuliza yeyote atakayekuwako ndani pembeni mwa nyumba, “Je kuna mtu mwingine pamoja nawe?” Naye atamjibu, “La! Hamna!” Naye atamwambia, “Nyamaza kimya! Tusilitaje hata jina la Mwenyezi-Mungu.”
11 Tazama! Mwenyezi-Mungu anatoa amri,nalo jumba kubwa labomoka vipandevipande,na nyumba ndogo kusagikasagika.