17 Afadhali mlo wa jioni wa mchicha na upendo,kuliko karamu ya nyama nono pamoja na chuki.
18 Mtu wa hasira mbaya husababisha ugomvi,lakini asiye mwepesi wa hasira hutuliza ugomvi.
19 Njia ya mvivu imesambaa miiba,njia ya mwaminifu ni wazi kama barabara kuu.
20 Mtoto mwenye hekima humfurahisha baba yake,lakini mpumbavu humdharau mama yake.
21 Upumbavu ni furaha kwa mtu asiye na akili,lakini mwenye busara huchagua njia iliyo sawa.
22 Mipango huharibika kwa kukosa shauri,lakini kwa washauri wengi, hufaulu.
23 Kutoa jibu sahihi hufurahisha;neno lifaalo kwa wakati wake ni jema mno!