24 Njia ya mwenye hekima huelekea juu kwenye uhai,ili aepe kuingia chini kuzimu.
25 Mwenyezi-Mungu huyabomoa makao ya wenye kiburi,lakini huilinda mipaka ya makao ya mjane.
26 Mawazo ya mwovu ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu,bali maneno mema humfurahisha.
27 Anayetamani faida ya ulanguzianaitaabisha jamaa yake,lakini achukiaye hongo ataishi.
28 Moyo wa mwadilifu hufikiri kabla ya kujibu,lakini kinywa cha mwovu hububujika uovu.
29 Mwenyezi-Mungu yuko mbali na watu waovu,lakini yu karibu na watu wema kuwasikiliza.
30 Macho ya huruma hufurahisha moyo,habari njema huuburudisha mwili.