12 Ni chukizo kubwa wafalme kutenda uovu,maana msingi wa mamlaka yao ni haki.
13 Mfalme hupendelea mtu asemaye kwa unyofu;humpenda mtu asemaye ukweli.
14 Hasira ya mfalme ni kama mjumbe wa kifo;mtu mwenye busara ataituliza.
15 Uso wa mfalme ukingaa kuna uhai;wema wake ni kama wingu la masika.
16 Kupata hekima ni bora kuliko dhahabu;kupata akili ni chaguo bora kuliko fedha.
17 Njia ya wanyofu huepukana na uovu;anayechunga njia yake huhifadhi maisha yake.
18 Kiburi hutangulia maangamizi;majivuno hutangulia maanguko.