1 Afadhali mkate mkavu kwa amani,kuliko karamu katika nyumba ya ugomvi.
2 Mtumwa mwenye busara atachukua nafasi ya mwana mpumbavu,atapata sehemu ya urithi wa jamaa hiyo.
3 Ubora wa dhahabu ama fedha hupimwa kwa moto,lakini Mwenyezi-Mungu ndiye apimaye mioyo ya watu.
4 Mtenda maovu husikiliza maneno mabaya,mwongo hutegea sikio ulimi mdanganyifu.
5 Anayemdhihaki maskini anamtukana Muumba wake;anayefurahia maafa hatakosa kuadhibiwa.
6 Wazee huwaonea fahari wajukuu zao;watoto huwaonea fahari wazazi wao.