16 Ya nini mpumbavu kuwa na fedha mkononi kununulia hekima,wakati yeye mwenyewe hana akili?
17 Rafiki wa kweli ni rafiki siku zote,ndugu huzaliwa asaidie wakati wa taabu.
18 Si jambo la akili kuweka rehani,na kuwa mdhamini wa mtu mwingine.
19 Anayependa ugomvi anapenda dhambi;anayejigamba anajitafutia maangamizi.
20 Mwenye moyo mpotovu hafanikiwi,na msema uongo hupatwa na maafa.
21 Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,na baba wa mpumbavu hana furaha.
22 Moyo mchangamfu ni dawa,bali moyo wenye huzuni hudhoofisha mwili.