23 Mtu mbaya hupokea hongo kwa siriili apate kupotosha haki.
24 Mtu mwenye busara lengo lake ni hekima,lakini mpumbavu hupania kila kitu duniani.
25 Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,na uchungu kwa mama yake mzazi.
26 Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia;ni kosa kumchapa viboko muungwana.
27 Asiyesema sana ana maarifa;mtu mtulivu ni mwenye busara.
28 Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.