25 Mtoto mpumbavu ni huzuni kwa baba yake,na uchungu kwa mama yake mzazi.
26 Si vizuri kumtoza faini mtu asiye na hatia;ni kosa kumchapa viboko muungwana.
27 Asiyesema sana ana maarifa;mtu mtulivu ni mwenye busara.
28 Hata mpumbavu akinyamaza huonekana ana hekima;akifunga mdomo wake huonekana kuwa mwenye akili.