1 Mwanangu, ukiyakubali maneno yangu,na kuyathamini maagizo yangu;
2 ukitega sikio lako kusikiliza hekima,na kuuelekeza moyo wako upate ufahamu;
3 naam, ukiomba upewe busara,ukisihi upewe ufahamu;
4 ukiitafuta hekima kama fedha,na kuitaka kama hazina iliyofichika;
5 hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu,utafahamu maana ya kumjua Mungu.
6 Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima;kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.