11 Busara itakulinda,ufahamu utakuhifadhi;
12 vitakuepusha na njia ya uovu,na watu wa maneno mapotovu;
13 watu waziachao njia nyofu,ili kuziendea njia za giza;
14 watu wafurahiao kutenda maovu,na kupendezwa na upotovu wa maovu;
15 watu ambao mienendo yao imepotoka,nazo njia zao haziaminiki.
16 Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati,mwanamke malaya wa maneno matamu;
17 mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake,na kulisahau agano la Mungu wake.