14 watu wafurahiao kutenda maovu,na kupendezwa na upotovu wa maovu;
15 watu ambao mienendo yao imepotoka,nazo njia zao haziaminiki.
16 Hekima itakuwezesha kumkwepa mwanamke mwasherati,mwanamke malaya wa maneno matamu;
17 mwanamke amwachaye mwenzi wa ujana wake,na kulisahau agano la Mungu wake.
18 Nyumba yake yaelekea kuzimu,njia zake zinakwenda ahera.
19 Yeyote amwendeaye kamwe harudi,wala hairudii tena njia ya uhai.
20 Kwa hiyo utafuata mfano wa watu wema,na kuzingatia mienendo ya waadilifu.