5 hapo utaelewa ni nini kumcha Mwenyezi-Mungu,utafahamu maana ya kumjua Mungu.
6 Maana Mwenyezi-Mungu huwapa watu hekima;kinywani mwake hutoka maarifa na ufahamu.
7 Huwawekea wanyofu akiba ya hekima safi,yeye ni ngao kwa watu waishio kwa uaminifu.
8 Huilinda mienendo ya watu watendao haki,na kuzihifadhi njia za waaminifu wake.
9 Ukinisikiliza utafahamu uadilifu na haki,utajua jambo lililo sawa na jema.
10 Maana hekima itaingia moyoni mwako,na maarifa yataipendeza nafsi yako.
11 Busara itakulinda,ufahamu utakuhifadhi;