1 Divai huleta dhihaka na kileo huleta ugomvi;yeyote anayevutiwa navyo hana hekima.
2 Ghadhabu kali ya mfalme ni kama simba angurumaye;anayemkasirisha anayahatarisha maisha yake.
3 Ni jambo la heshima kuepa ugomvi;wapumbavu ndio wanaogombana.
4 Mvivu halimi wakati wa kulima;wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.
5 Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji;lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo.