12 Sikio lisikialo na jicho lionalo,yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.
13 Usipende kulala tu usije ukawa maskini;uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.
14 “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika,lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.
15 Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa;lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!
16 Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni,chukua nguo yake;mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.
17 Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.
18 Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.