15 Kuna dhahabu na wingi wa mawe ya thamani kubwa;lakini cha thamani kubwa zaidi ni maneno ya busara!
16 Mtu akiahidi mbele yako kumdhamini mgeni,chukua nguo yake;mfanye awajibike kwa kuwadhamini wageni.
17 Chakula kipatikanacho kwa udanganyifu ni kitamu,lakini baadaye huwa kama mchanga kinywani.
18 Mipango mizuri hufanyika kwa kushauriana;ukitaka kuanza vita lazima kutafakari kwanza.
19 Mpiga domo hafichi siri,kwa hiyo mwepe mtu wa kuropoka.
20 Anayemlaani baba yake au mama yake,mwanga wa uhai wake utazimwa kama taa gizani.
21 Mali iliyopatikana kwa haraka mwanzoni,haitakuwa ya heri mwishoni.