4 Mvivu halimi wakati wa kulima;wakati wa mavuno atatafuta asipate chochote.
5 Fikira za mtu zimefichika kama kilindi cha maji;lakini mtu mwenye busara ajua kuzichota humo.
6 Watu wengi hujivunia kuwa wema,lakini mwaminifu wa kweli apatikana wapi?
7 Mtu mwadilifu akiishi kwa unyofu;watoto wake atakaowaacha watabarikiwa.
8 Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu,huupepeta uovu wote kwa macho yake.
9 Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu;mimi nimetakasika dhambi yangu?”
10 Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu,vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.