8 Mfalme mwema aketipo kutoa hukumu,huupepeta uovu wote kwa macho yake.
9 Nani athubutuye kusema: “Nimeutakasa moyo wangu;mimi nimetakasika dhambi yangu?”
10 Mizani ya udanganyifu na vipimo vya udanganyifu,vyote ni chukizo kwa Mwenyezi-Mungu.
11 Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake,kama tabia yake ni njema na aminifu.
12 Sikio lisikialo na jicho lionalo,yote mawili kayafanya Mwenyezi-Mungu.
13 Usipende kulala tu usije ukawa maskini;uwe macho nawe utakuwa na chakula kingi.
14 “Hakifai, hakifai”, mnunuzi hulalamika,lakini akiondoka hujisifu amepunguziwa bei.