1 Moyo wa mfalme ni kama maji yanayotiririka;Mwenyezi-Mungu, huuongoza popote apendapo.
2 Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake,lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo.
3 Kutenda mambo mema na ya haki,humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko.
4 Macho ya kiburi na moyo wa majivunohuonesha wazi dhambi ya waovu.
5 Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi,lakini kila aliye na pupa huishia patupu.