17 Anayependa anasa atakuwa maskini;anayefikiria tu kula na kunywa hatatajirika.
18 Mwovu atapata pigo ambalo halitampata mtu mwema,mkosefu ataadhibiwa badala ya mnyofu.
19 Afadhali kuishi jangwani,kuliko kukaa na mwanamke mgomvi na msumbufu.
20 Nyumbani kwa mwenye busara mna hazina za thamani,lakini mpumbavu huponda mali yake yote.
21 Anayepania uadilifu na huruma,ataishi maisha marefu na kuheshimiwa.
22 Mwenye hekima aweza kuteka mji wa wenye nguvu,na kuziporomosha ngome wanazozitegemea.
23 Achungaye mdomo wake na ulimi wake,hujiepusha na matatizo.