2 Matendo yote ya mtu ni sawa machoni pake,lakini Mwenyezi-Mungu hupima mioyo.
3 Kutenda mambo mema na ya haki,humpendeza Mwenyezi-Mungu kuliko tambiko.
4 Macho ya kiburi na moyo wa majivunohuonesha wazi dhambi ya waovu.
5 Mipango ya mtu wa bidii huleta mali kwa wingi,lakini kila aliye na pupa huishia patupu.
6 Mali ipatikanayo kwa udanganyifu,ni mvuke upitao na mtego wa kifo.
7 Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali,maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki.
8 Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka,lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka.