22 Mwenye hekima aweza kuteka mji wa wenye nguvu,na kuziporomosha ngome wanazozitegemea.
23 Achungaye mdomo wake na ulimi wake,hujiepusha na matatizo.
24 Mwenye majivuno na kiburi jina lake ni “Madharau;”matendo yake yamejaa majivuno ya ufidhuli wake.
25 Mvivu hufa kwa kutotimizwa tamaa zake,maana mikono yake milegevu haitaki kufanya kazi.
26 Mchana kutwa mwovu hutamani kupata kitu,lakini mwadilifu hutoa, tena kwa ukarimu.
27 Tambiko ya mwovu ni kitu cha kuchukiza,huchukiza zaidi akiitoa kwa nia mbaya.
28 Shahidi mwongo ataangamia,lakini msikivu hawezi kunyamazishwa.