6 Mali ipatikanayo kwa udanganyifu,ni mvuke upitao na mtego wa kifo.
7 Ukatili wa wakatili utawafutilia mbali,maana wanakataa kutenda yaliyo ya haki.
8 Njia ya mtu mwenye hatia imepotoka,lakini mwenendo wa mnyofu umenyooka.
9 Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi.
10 Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu;hata kwa jirani yake hana huruma.
11 Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima;ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa.
12 Mungu Mwadilifu anajua wanayotenda waovu nyumbani kwao;naye atawaangusha na kuwaangamiza.