9 Afadhali kuishi pembeni juu ya paa,kuliko kuishi nyumbani na mwanamke mgomvi.
10 Anachopania kutenda mtu mbaya ni uovu;hata kwa jirani yake hana huruma.
11 Ukimwadhibu mwenye dhihaka, mjinga hupata hekima;ukimfundisha mwenye hekima, unampatia maarifa.
12 Mungu Mwadilifu anajua wanayotenda waovu nyumbani kwao;naye atawaangusha na kuwaangamiza.
13 Anayekataa kusikiliza kilio cha maskini,naye pia hatasikilizwa atakapolilia msaada.
14 Hasira hutulizwa kwa zawadi ya siri;tunu apewayo mtu imefichwa hupooza ghadhabu.
15 Haki ikitekelezwa watu wema hufurahi,lakini watu waovu hufadhaishwa.