14 Kinywa cha mwasherati ni shimo refu;anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.
15 Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni,lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo.
16 Anayemdhulumu maskini atamfanya afaidike mwishowe,anayewapa matajiri zawadi ataishia kuwa maskini.
17 Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima,elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu.
18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni,na kuyakariri kila wakati.
19 Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.
20 Nimekuandikia misemo thelathini,misemo ya maonyo na maarifa,