17 Tega sikio usikie maneno ya wenye hekima,elekeza moyo wako uzingatie maarifa yangu.
18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni,na kuyakariri kila wakati.
19 Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.
20 Nimekuandikia misemo thelathini,misemo ya maonyo na maarifa,
21 ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli;na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.
22 Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini,wala usimnyime fukara haki yake mahakamani.
23 Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea;atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu.