18 Wewe utafurahi endapo utayaweka moyoni,na kuyakariri kila wakati.
19 Ninayependa kumfundisha leo ni wewe,ili tegemeo lako liwe kwa Mwenyezi-Mungu.
20 Nimekuandikia misemo thelathini,misemo ya maonyo na maarifa,
21 ili kukufundisha yaliyo sawa na kweli;na mtu akikuuliza uweze kumpa jibu sahihi.
22 Usimdhulumu maskini kwa kuwa ni maskini,wala usimnyime fukara haki yake mahakamani.
23 Maana Mwenyezi-Mungu atawatetea;atawapokonya maisha yao wale watakaowadhulumu.
24 Usifanye urafiki na mtu wa hasira,wala usiandamane na mwenye ghadhabu,