6 Mfunze mtoto namna ya kuishi vizuri,naye hatasahau njia hiyo hata uzeeni.
7 Tajiri humtawala maskini;mkopaji ni mtumwa wa mkopeshaji.
8 Apandaye dhuluma atavuna janga;uwezo wake wa kutenda mabaya utavunjwa.
9 Mtu mkarimu atabarikiwa,maana chakula chake humgawia maskini.
10 Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka,ugomvi na matusi vitakoma.
11 Mwenye nia safi na maneno mazuri,atakuwa rafiki wa mfalme.
12 Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli,lakini huyavuruga maneno ya waovu.