9 Mtu mkarimu atabarikiwa,maana chakula chake humgawia maskini.
10 Mfukuze mwenye dharau na fujo itatoweka,ugomvi na matusi vitakoma.
11 Mwenye nia safi na maneno mazuri,atakuwa rafiki wa mfalme.
12 Mwenyezi-Mungu hulinda elimu ya kweli,lakini huyavuruga maneno ya waovu.
13 Mvivu husema, “Siwezi kutoka nje;kuna simba huko, ataniua!”
14 Kinywa cha mwasherati ni shimo refu;anayechukiwa na Mwenyezi-Mungu atatumbukia humo.
15 Mtoto hupenda mambo ya kijinga moyoni,lakini fimbo ya nidhamu humwondolea hayo.