11 Mwokoe mtu anayechukuliwa kuuawa bure;usisite kumwokoa anayeuawa bila hatia.
12 Usiseme baadaye: “Hatukujua!”Maana Mungu apimaye mioyo ya watu huona;yeye atakulipa kulingana na matendo yako!
13 Mwanangu, ule asali maana ni nzuri;sega la asali ni tamu mdomoni.
14 Ndivyo ilivyo hekima nafsini mwako;ukiipata utakuwa na matazamio mema,wala tumaini lako halitakuwa la bure.
15 Usivizie kama mwovu kushambulia makao ya mtu mwema,wala usijaribu kuiharibu nyumba yake,
16 maana mtu mwema huanguka mara nyingi lakini huinuka,lakini mtu mwovu huangamizwa na janga.
17 Usishangilie kuanguka kwa adui yako;usifurahie moyoni mwako kujikwaa kwake,