2 maana fikira zao zote ni juu ya ukatili,hamna jema lolote litokalo midomoni mwao.
3 Nyumba hujengwa kwa hekima,na kuimarishwa kwa busara.
4 Kwa maarifa vyumba vyake hujazwavitu vya thamani na vya kupendeza.
5 Kuwa na hekima ni bora kuliko kuwa na nguvu,naam, maarifa ni bora kuliko nguvu.
6 Maana kwa mwongozo mzuri waweza kupigana vita,na kwa washauri wengi ushindi hupatikana.
7 Kwa mpumbavu hekima ni ngumu kuielewa;penye mkutano wa mashauri hafungui mdomo.
8 Afikiriaye kutenda maovu daimaataitwa mtu mwenye fitina.