5 Mwenye kumbembeleza jirani yake,anatega mtego wa kujinasa mwenyewe.
6 Mtu mbaya hunaswa kwa kosa lake,lakini mtu mwadilifu huimba na kufurahi.
7 Mwadilifu anajua haki za maskini,lakini mtu mwovu hajui mambo hayo.
8 Wenye dharau huutia vurugu mji mzima,lakini wenye hekima hutuliza ghadhabu.
9 Mwenye hekima akibishana na mpumbavu,mpumbavu huwaka hasira na kucheka bila kutulia.
10 Wapendao kumwaga damu humchukia mtu asiye na hatia,lakini watu wema huyalinda maisha yake.
11 Mpumbavu huonesha hasira yake wazi,lakini mwenye hekima huizuia na kuituliza.