1 Mwanangu, usiyasahau mafundisho yangu,bali kwa moyo wako uzishike amri zangu.
2 Maana yatakupa wingi wa siku,maisha marefu na fanaka kwa wingi.
3 Utii na uaminifu visitengane nawe.Vifunge shingoni mwako;viandike moyoni mwako.
4 Hivyo utakubalika na kusifika,mbele ya Mungu na mbele ya wanadamu.