14 Hekima ni bora kuliko fedha,ina faida kuliko dhahabu.
15 Hekima ina thamani kuliko johari,hamna unachotamani kiwezacho kulingana nayo.
16 Kwa mkono wake wa kulia Hekima atakupa maisha marefu;kwa mkono wake wa kushoto atakupa mali na heshima.
17 Njia zake ni za kupendeza,zote zaelekea kwenye amani.
18 Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;wana heri wote wanaoshikamana naye.
19 Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,kwa akili aliziimarisha mbingu.
20 Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,na mawingu yakadondosha umande.