18 Hekima ni mti wa uhai kwa wote wampatao;wana heri wote wanaoshikamana naye.
19 Kwa hekima Mwenyezi-Mungu aliweka misingi ya dunia,kwa akili aliziimarisha mbingu.
20 Kwa maarifa yake vilindi vilipasuka,na mawingu yakadondosha umande.
21 Mwanangu, zingatia hekima safi na busara;usiviache vitoweke machoni pako,
22 navyo vitakuwa uhai nafsini mwako,na pambo zuri shingoni mwako.
23 Hapo utaweza kwenda zako kwa usalama,wala mguu wako hautajikwaa.
24 Ukiketi hutakuwa na hofu;ukilala utapata usingizi mtamu.